Tukio hilo lililotokea majira ya saa tano usiku huko Mwananyamala mtaa wa Kopa wilaya ya Kinondoni , huku ikidaiwa kwamba kijana aliyeuwa alifika nyumbani kwao na kubwata kwa wapangaji kwamba hawalipi umeme ndipo mpangaji mmoja ambaye ndiye baba wa marehemu mwenye asili ya Kimalawi aliamua kumtuliza kijana huyo ili aache kubwata na kutoa matusi.
Baada ya taarifa hizo Supamix ilitia timu mpaka kwenye eneo la tukio na kuzungumza na wahusika ambapo mashuda wa tukio hilo wamesema kwamba kijana huyo alipofika alidai kwamba kuna watu ambao hawakununua umeme hivyo kuanza kusumbua wapangaji, na Marehemu Wilson kuingilia baada ya kuona baba yake anasukumwa hali iliyopelekea huyo kijana wa mwenye nyumba kuchukua kisu ndani na kumchoma mwenzake.
Aidha Shuhuda wa Tukio hio amesema kwamba baada ya tukio hilo Kijana aliyechomwa kisu aliondoka akikimbia kutokana na maumivu na kuangukia mbali kidogo na nyuma hiyo hali iliyopelekea mpita njia kutoa taarifa baada ya kuona damu zinamtoka na hata apochukuliwa kwa ajili ya kufikishwa hospitali alifariki akiwa njiani.
Hata hivyo Supamix ilizungumza na mama mzazi wa kijana aliyefanya tukio hilo ambaye naye kwa masikitiko anasema kwamba kijana wake alianza kulalamika kuhusu kulala giza lakini anadai alimnyamazisha na kumtaka aingie ndani lakini pia anawaachia serikali ichukue hatua juu ya tukio lililotokea.
Baada ya kutoka nyumbani Supamix ilifunga safari mpaka Hospital ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala na kumkukuta baba mzazi wa marehemu akilia kwa uchungu na hapa anaelezea hali halisi. Msikilize hapa




