Ijumaa , 28th Feb , 2014

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Rufftone anatarajia kwenda huko nchini Korea kwa ajili ya kozi fupi kujifunza lugha pamoja na utamaduni wa watu wa huko, kozi ambayo itachukua takriban miezi miwili mpaka kukamilika kwake.

Rufftone amepata nafasi hii akiwa kama Balozi wa Mahusiano Mema wa nchi ya Korea, na atakwenda huko na timu ya watu kadhaa kama programu ya kubadilishana ujuzi, ambayo pia itatuma timu ya watu kutoka Korea kuja nchini Kenya kujifunza utamaduni wake.

Nafasi hii adhimu inamuongezea msanii huyu wigo wa ufahamu ambao pia utakua na manufaa makubwa kwake akiwa kama msanii wa muziki.