
P Funk Majani amesema hayo baada ya wakali hao jana kufanikiwa kufanya ngoma inayokwenda kwa jina la 'Mvua' ambayo P Funk Majani anaamini kazi hiyo itakuja kuleta mapinduzi kwenye muziki wa hip hop na kuja kuwashusha MCs waliojuu sasa.
"Fid Q kuanzia jana wewe umekuwa rasmi MC namba moja kwangu duniani, maana umetisha sana, huu ni wakati sahihi kusema bye bye kwa huyu top (mnafiki) unaweza kuwa juu lakini huwezi kuwa mkali kama Fid Q" alisema P Funk Majani
Kwa upande wake Fid Q alimshukuru sana P Funk Majani kwanza kwa kuweza kutambua na kuthamini kipaji chake na kuweza kumtengenezea ngoma hiyo ya 'Mvua' na kusema tangu alipoamka asubuhi amekuwa akiisikiliza kazi hiyo tu.
Pia Fid Q alisema kuwa amefurahi kusikia maneno hayo kutoka kwa mkongwe wa muziki ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika muziki wa bongo fleva, ambaye ameweza kubadili muziki wa hip hop kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine.