Dj huyo ambaye alilelewa kwenye maisha yenye maadili ya dini huku mama yake akiwa ni mwana kwaya kanisani, alijitahidi kupigania muziki wa bongo fleva wakati unaanza nchini Tanzania, kwa kuwashika mkono wasanii mbali mbali, mpaka kufikia hatua ya kuwa wasanii wakubwa na kuitangaza bongo fleva.
Dj Bony Love ambaye kwa sasa na umri wa miaka 46 , ametumia zaidi ya miaka 31 katika maisha yake katika tasnia ya muziki ikiwemo u-Dj na uandaaji wa muziki (producer), tangu bongo fleva inazaliwa na kuweza kusimama.
Dj Bonny Love alitumia muda, akili na nguvu zake katika kuinua sanaa ya Tanzania, kwa kutafuta wasanii na kuwapa fursa ya kurekodi bure, huku wasanii wengi wakubwa kwenye game ya bongo fleva wamepitia mikononi mwake, wakiwemo Juma Nature ambaye ndiye msanii anayesimama kama icon ya muziki wa bongo fleva, King Crazy Gk, mwana FA, Ay na wengineo.
Pia Dj Bonny love ni kaka wa maDj wakubwa wawili hapa bongo, wakiwemo Dj Venture na Dj Mackay. Tazama historia yake hapa chini