Jumatano , 14th Mei , 2014

Rapa Rabbit aka Kaka Sungura kutoka nchini Kenya, ametoa maneno ya shukrani kwa mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Facebook, kuwajulisha namna anavyowathamini na kuelewa mchango wao katika kumfikisha alipo sasa.

Rabbit

Rapa huyu amesema hayo ikiwa ni sehemu ya kufurahia familia ya mashabiki wake kupitia mtandao kuendelea kuwa kubwa na pia kwa kazi zake kuendelea kusambaa na kukubalika katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Msanii huyu ameweka wazi kuwa, kumekuwa na hatua kubwa katika muziki wake tangu mwaka 2008 alipotoka na kazi inayokwenda kwa jina "Niko kwa Jam Nakam", mpaka sasa ambapo amefanikisha kutengeneza project kubwa kama Ligi Soo,Tulia Tu na nyinginezo ambazo zinaendelea kufanya poa.

Tags: