Jumanne , 29th Nov , 2016

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoa wa Mtwara imekanusha taarifa zilizoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa bandari hiyo imezidiwa na kushindwa kumudu kusafirisha kikamilifu zao la korosho.

Bandari ya Mtwara

 

Akizungumza Bandarini hapo, Afisa Utekelezaji Mwandamizi wa Bandari hiyo Robert Soko, amesema licha ya kuwa na uwezo wa kupakia idadi ya kontena 200 kwa siku, lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa mizigo, hivyo kushindwa kuifikia idadi hiyo.

Aidha, amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa wasafirishaji kutopeleka mizigo kwa wakati, hali inayosababisha baadhi ya meli kulazimika kusafiri bila kuwa na mzigo wa kutosha.

Bandari hiyo tayari imesafirisha jumla ya Tani 34,500 za korosho, tangu ulivyoanza msimu wa ununuzi wa zao hilo.