Wawakilishi kutoka EATV, Baclays, BASATA, Vodacom na Innovate katika mkutano na wanahabari.
Kupitia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, EATV LTD ikishirikana na Vodacom Tanzania, CocaCola, Barcklays Bank, kampuni ya ukaguzi ya Innovate pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) imetaja vipengele hivyo vitatu, ambavyo ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki bora wa kike na wimbo bora wa mwaka.
Godfrey Mngereza - Katibu Mtendaji wa BASATA
Wasanii hao tukianzia na msanii bora wa kiume ni
G Nako - 'Original'
Shetta - 'Namjua'
Ben Pol - 'Moyo Mashine'
Mwana FA - 'Ahsanteni kwa kuja'
Alikiba - 'Aje'
Kipengele kingine ni mwanamuziki bora wa kike, ambapo wasanii waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro ni
Lilian Mbabazi - 'Yoola' (Uganda)
Ruby - 'Forever'
Linah - 'Malkia wa nguvu'
Vanessa Mdee - 'Never ever'
Lady Jaydee - 'NdiNdiNdi'
Kipengele cha mwisho ambacho kilitangazwa washiriki wake leo kilikuwa ni wimbo bora wa mwaka, na nyimbo zilizofanikiwa kuingia ni kama ifuatavyo:
Don't Bother - Joh Makini
NdiNdiNdi - Lady Jayde
Kamatia chini - Navy Kenzo
Aje - Alikiba
Moyo Mashine - Ben Pol
Baada ya kutangazwa kwa vipengele hivyo tayari zoezi upigaji kura limefunguliwa kuanzia leo saa sita usiku kwa njia ya simu kupitia namba 15777 na njia ya mtandao kupitia tovuti ya eatv.tv/awards kwa utaratibu utakaotangazwa.
Zoezi hilo la upigaji kura litakamilika tarehe 8/12/2016.