
Rais Dkt. John Magufuli akifanya ukaguzi katika eneo la Gati la Mafuta la Kurasini KOJ.
Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa kati ya mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo, ni mashine mbili pekee ndizo zinafanya kazi na hazina uwezo wa kukagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini kupitia bandari hiyo hali inayosababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakika wa udanganyifu.
Dkt. Magufuli ameiagiza (TPA) kwa kushirikiana na wizara husika kuanza mazungumzo na kampuni ya kimataifa ya kuhudumia shehena ya makasha bandarini (TICTS) ambayo inapakia na kupakua mizigo katika gati namba nane hadi kumi na moja ili kurekebisha mkataba ya mafuta yanayopakuliwa melini.
Ameiagiza TPA kuharakisha mchakato wa kununua mita mpya (Flow Meters) na kuzifunga.

