
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuurugenzi Mkuu wa Chama hicho Bi. Edda Sanga, amewataka wadau wa usalama barabarani kuadhimisha wiki ya usalama barabarani kwa kupaza sauti na kutoa wito wa kufanyiwa marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarani ya mwaka 1972.
Bi. Edda Sanga ameyataja maeneo yanayopaswa kufanyiwa kazi kuwa ni pamoja na marekebisho katika sheria za Mwendokasi, ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi vya watoto.
Mkurugenzi huyo ametoa takwimu zinazoonesha kuwa watu 1580 walifariki dunia kutokana na ajali za barabarani katika kipindi cha miezi saba kuanzia Januari hadi Julai mwaka huuu ikiwa ni wastani wa watu saba kila siku.