Jumatatu , 12th Sep , 2016

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema linafuatilia shindano la Dance100% kwa makini ili kuona vipaji vya vijana pamoja na kuhakikisha haki inatendeka kwa makundi yanayoshiriki shindano hilo.

Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Kurwijira N. Maregesi

Akizungumza na makundi yaliyofuzu hatua ya fainali Jijini Dar es Salaam Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Kurwijira N. Maregesi amesema sanaa ni ajira na BASATA kama msimamizi wa shughuli za sanaa wameona ni vyema wakashiriki kikamilifu katika hatua zote za shindano ili kuona haki inatendeka.

“Kundi litashinda kutokana na namna litakavyoonesha ubunifu pamoja na mambo ambayo mmeelekezwa na majaji na katika makubaliano yenu ya ushiriki, hivyo hakuna kundi litakalopendelewa, haki itatendeka hivyo kajiandaeni kwa hari mkijua mshindi atapatikana kadri ya kazi atakayoonyesha” Amesema Maregesi wakati akiyapa maelekezo makundi

Shindano la Dance100% linaendeshwa na EATV na kudhaminiwa na VODACOM na COCA -COLA na kuonyeshwa na EATV kila Jumapili saa moja jioni.

Tags: