Jumatano , 19th Feb , 2014

Mrembo Dilish Mathews kutoka Namibia, baada ya kukiri kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Stephen Gaeseb, kwa sasa ameonyesha kuwa karibu sana na staa wa muziki wa Nigeria Flavour, katika kila dalili inayoonyesha kuwepo kwa mahusiano ya kimapenzi kati yao.

Mrembo huyu ametajwa kupagawisha hisia za Flavour kwa muda sasa, mpaka kufikia hatua ya msanii huyu kuamua kumshirikisha katika video yake mpya Ikworikwo, na tangu hapo urafiki na ukaribu wao umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Flavour tayari amekwishaanza kuweka picha ya mtandaoni akiwa katika wakati mzuri pamoja na Dilish ambaye yeye binafsi kwa sasa anamuita kwa jina 'Mama'a.