
Katika sakata hili, Juma Seiko pamoja na John Kaddu wamejitambulisha kama baba halali wa binti huyu wa Desire ambaye kwa sasa miaka 10, na kwa mujibu wa waalimu wa shule ambayo anasoma binti huyu, John Kaddu ndiye anayetambulika kama baba wa binti huyu, ambapo amekuwa akifuatilia maendeleo yake shuleni kwa karibu.
Desire bado hajalitolea ufafanuzi suala hili, na kwa upande wa Juma Seiko, amesema kuwa yupo tayari kwa vipimo vya DNA, huku Kaddu akiweka wazi kuwa mama wa mtoto huyu ndiye anayefahamu ukweli na anatakiwa kuweka wazi kuhusiana na ukweli juu ya baba wa mtoto.