Jumatatu , 5th Mei , 2014

Kundi la muziki la Goodlyfe linaloundwa na Radio pamoja Weasel wamefanikiwa kuweka historia ya aina yake katika onyesho lao la Amaaso-Ntunga lililofanyika mwishoni mwa wiki huko Kampala Uganda, ambapo mastaa kibao na mashabiki walijitokeza kuwasapoti

Goodlyfe

Kivutio kikubwa katika onyesho hili, ilikuwa ni aina ya uingiaji wa wasanii hawa katika jukwaa, ambapo walitumia winch kuwashusha jukwaani, vile vile umoja ulioonyeshwa na wasaniiBobi Wine, Bebe Cool, Desire, Iryn Namubiru pamoja na wengineo ambao walipanda jukwaani kutumbuiza.

Kwa njia ya mtandao, Moze Radio amesema kuwa, anawashukuru mashabiki kwa moyo na upendo waliionyesha katika shoo hii, licha ya tyaarifa mbalimbali zilizokuwa zinasambazwa na mahasimu wao ili kuharibu show hii iliyofanyika kwa mafanikio makubwa.

Tags: