Alhamisi , 4th Aug , 2016

Mkaguzi Mkuu wa nje wa Hesabu za Serikali Mkoani Morogoro, Peter Mwambanga amesema kuwa halmashauri ya Morogoro inatakiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na benki inazozitumia kulipa mishahara ya watumishi wa halmashauri hizo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene

Mkaguzi Mkuu huyo amesema kuwa kutokuwepo kwa mawasaliano baina ya pande hizo mbili kumekuwa kukichangia malipo kwa watumishi hewa ambapo katika mwaka wa fedha 2015/2016 zaidi ya shilingi milioni 42 zimelipwa kwa watumishi hewa ndani ya manispaa ya Morogoro pekee yake.

Hayo yamebainika kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo licha ya kupewa ushauri juu ya suala hilo lakini manispaa hiyo imepata hati safi na kuwa miongoni mwa halmashauri 47 zilizopata hati safi.

Awali akifungua kikao hicho Maalumu cha baraza la madiwani Kaimu katibu Tawala
Msaidizi TAMISEMI, Noel Kazimoto, amewasisitiza wakuu wa idara kuhakiki taarifa za watumishi ili kuepuka kulipa mishahara kwa watumishi hewa.