Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
Maadhimisho hayo ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika nje ya Jiji la Dar es Salaam, mkoani Dodoma ambapo Rais Magufuli amesema hiyo ni ni moja ya harakati zake za kuhamishia serikali Mkoani Dodoma ndani ya miaka minne ya Muhula wake wa kwanza.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Rais Magufuli, amesema mpaka sasa Dodoma, imeshakua na miundombinu ya kutosha ya kuweza kumudu watumishi wote wa wizara zake hivyo atakafanya kila awezalo ili serikali ihamie mkoani humo haraka iwezekanavyo.
Aidha Rais Magufuli amesisitiza kauli yake ya kuwatumikia wa Watanzania bila kujali itikadi zao za vyama na kusema kila mtanzania anahitaji haki sawa na kuondokewa na kero mbalimbali zinazowafanya kushindwa kufanya maendeleo
Pia Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania kutumia maadhimisho hayo ya siku ya Mashujaa kudumisha Amani na Umoja na kujenga uzalendo wa nchi kama walivyofanya mashujaa waliokufa katika vita kwa ajili ya kuletetea taifa.
Kwa upande wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, amewataka Watanzania wampe ushirikiano Rais Magufuli katika dhima yake ya kuwatumikia wananchi ikiwemo kumuombea kutekeleza yale yote ambayo aliwaahidi wakati wa kampeni.