Jumamosi , 23rd Jul , 2016

Klabu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara imesema, inaamini kikosi kilichokisajili kuelekea msimu ujao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara kinaiwezesha timu hiyo kuleta ushindani kwa timu nyingine.

Afisa habari wa Ndanda FC Idris Bandari amesema, wamesajili kwa kungalia nafasi zilizokuwa na mapungufu msimu uliopita hivyo wanaamini wachezaji hao wataisaidia timu kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

Wachezaji baadhi walioongeza mkataba na wengine waliosajili na kikosi cha Ndanda kwa ajili ya Maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara ni:

Makipa:

Jeremia Kisubu
Jackson Chove

Walinzi
Paul Ngalema
Aziz Sibo
Hemed Khoja

Viungo

William Lucian

Winga

Salum Minelly
Kigi Makasi

Washambuliaji

Omary Mponda
Riphati Hamis

Wachezaji wapya
Isihaka Hassan – Kiungo
Bem Slevester- Kiungo
Bakary Mtama - Mlinzi