Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Nchi za Afrika zinapaswa kuongeza wigo wa vyanzo vya mapato ili kufadhili maendeleo yao, la sivyo utegemezi wa mikopo utakwamisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu maendeleo ya kiuchumi barani Afrika iliyozinduliwa leo Nairobi, Kenya na kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Akizindua ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi ametaja vyanzo hivyo ni pamoja na pesa zinazotumwa na waafrika walio ughaibuni, udai kati ya sekta binafsi na umma na kuhakikisha zinadhibiti usafirishaji haramu wa fedha.

Mwandishi wa ripoti hiyo, Junior Roy Davis amesema Kenya iko mbele zaidi katika kurahisisha wale walioko ughaibuni kutuma fedha nyumbani na hivyo kujipatia kipato.

UNCTAD inasema utumaji fedha kutoka ughaibuni kwa mwaka ni dola bilioni 63 za kimarekani, kiwango cha juu zaidi kuliko hata misaada ya kigeni.