Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Hatua hiyo ya rais imekuja baada ya kupata taarifa ya Mhasibu wa jeshi la Polisi aliyesimamishwa kutokana na ubadhilifu wa malipo hewa kwa jeshi la polisi kuwa huenda hakuwa na taaluma yoyote ya upolisi.
Rais Magufuli ameliambia jeshi hilo endapo wanaona raia waliokuwa nao ndani ya jeshi hilo wanaliyumbisha jeshi wawapeleke ofisi za utumishi kwa ajili ya kuwapangia kazi nyingine ili jeshi la polisi libaki na watu waliopitia chuo cha polisi pekee.
Aidha rais Magufuli amesema ameshangazwa na jeshi la Polisi pamoja na taaluma zao za upelelezi pamoja na kuwa na ofisi ya upelelezi makao makuu lakini bado jeshi hilo lilishindwa kumkamata mtumishi huyo ambaye alikuwa analiibia jeshi hilo na serikali kwa Ujumla.
Rais Magufuli amesema kuwa kuna nafasi ambazo baadhi ya raia wanazishikilia wapo polisi ambao wamezisomea na wanaweza kuzimudu hivyo hakuna haja ya kuendelea kukaa na rais ndani ya jeshi la polisi ambao baadhi yao wanalitia doa jeshi hilo.