Naibu Waziri ameyasema hayo alipokuwa akiadhimisha siku ya ushirika iliyofanyika mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa vyama vya ushirika mkoani humo
''Vyama vya ushirika vimedidimia kutokana na siyo wanachama bali viongozi kuwalimbikizia madeni wanachama na wao kujilimbikizia mali huku vyama vikielekea kaburini''- Amesema Naibu Waziri Nasha.
Aidha Naibu waziri amewatahadharisha viongozi wa vyama vya ushirika nchini kwamba serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafilisi viongozi wote watakaobainika kuhujumu vyama vyao na wao kujilimbikia mali za ushirika.



