
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge Asha Abdula Juma aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutatua migogoro ya jeshi na wananchi wanaozunguka kambi hizo.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Dkt. Kigwangalla amesema kwamba serikali imejipanga vyema katika kutatua migogoro hiyo kwa kutaka kambi zipande miti ya kuzunguka kambi zao, kuweka uzio wa waya pamoja na mabango ya tahadhari.
''Jeshi limekuwepo kwenye maeneo hayo kwa muda mrefu, wananchi ndiyo mara nyingi huwafuata wengine kwa kujua na wengine pasipokujua jambo ambalo baadaye huzua migogoro hivyo nawasihi wananchi wasiendelee kusogeza mipaka''- amesema Kigwangalla.
Aidha Naibu Kigwangalla akijibu maswali kwa niaba ya jeshi la ulinzi na kujenga taifa amesema serikali imejenga maghala ya kuhifazia silaha na kuwahamisha mabomu na vilipuzi ili kuondokana na hali iliyotokea Gongo la Mboto na Mbagala kwa mabomu kulipuka na kuathiri maisha na mali.