Ijumaa , 17th Jun , 2016

Msanii wa Hip Hop aliyewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa 'siku nzuri inavyokwenda' nyingine nyingi Dani msimamo, ameamua kuvunja ukimya na kusema kwa sasa anajishughulisha na kilimo.

Dani Msimamo

Dani amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa kinamlipa zaidi na kumfanya michongo yake ya maisha iendelee.

Hata hivyo amewasihi wanamuziki wenzake kuwa na michongo mingine nje ya game ili kuweza kukimbizana na harakati za maisha na kuweza kuepuka vishawishi vinavyojitokeza hadi kupelekea baadhi ya wasanii kujiingiza katika madawa ya kulevya.