Ijumaa , 17th Jun , 2016

Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto imewataka wagonjwa wa sickle Cell waliokuwa wakitibiwa katika Hosptali ya taifa Muhimbili kuhudhuria katika vituo vilivyopo kwenye hosptali za mikoa na wilaya kwa ajili ya matibabu.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya siko cell duniani, Mkurugenzi kutoka kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii. Jinsia na watoto Prof. Ayub Magimba amesema kwa sasa Muhimbili inatoa huduma kwa wagonjwa wenye rufaa pekee.

Prof. Magimba amekanusha taarifa kuwa hosptali ya taifa Muhimbili aitoi tena huduma kwa wagonjwa hao, bali mradi wa kutoa huduma bure uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi binafsi umemalizika hivyo huduma inapatikana katika vituo vya afya vya mikoa na wilaya.

“Si kweli kuwa Muhimbili imewafukuza wagonjwa wa Sikle Cell, tuna wajali sana, ni mradi tuu umemalizika lakini huduma zitolewazo muhimbili kwa sasa nikwaajili ya wagonjwa wenye matatizo makubwa yatokanayo na Sickle Cell”amesema Prof. Magimba

Prof. Magimba amesema serikali inatambua garama zilizopo katika matibabu ya ugonjwa huo ambapo amewashauri wagonjwa wa Sikle Cell kuhakikisha kuwa wanakuwa na bima ya afya ili kumudu garama za matibabu ya ugonjwa huo.