Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Stand United Muhibu Kanu amesema, licha ya wachezaji walio ndani ya kikosi lakini pia wapo wachezaji walio ndani ya vilabu vingine vya Ligi kuu ambao wameshaliza mikataba yao.
Kanu amesema, usajili huo unatokana na ripoti ambayo Kocha Patrick Liewing aliiwasilisha kwa kuelezea mapungufu ndani ya timu na kipi kinahitajika kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa ajili ya ushindani msimu ujao.
Kanu amesema, wanatarajia mpaka Ijumaa ya Julai 17 watakuwa wameshakamilisha zoezi zima la kuchagua wachezaji ambao watakuwa nao kwa msimu ujao wa Ligi Liu ya Soka Tanzania Bara 2016/17.
Kwa upande mwingine Kanu amesema, hawaangalii wachezaji pekee kwa ajili ya kuboresha kikosi lakini pia wapo katika mchakato wa kuweza kuboresha benchi is ufundi ili kuweza kuleta ushindani katika msimu ujao wa Ligi na kufikia malengo waliyojiwekea.
Kanu amesema, mara baada ya kumaliza zoezi zima la kutengeneza timu na benchi la ufundi wataanza maandalizi ya msimu ujao wa Ligi.