Chama cha United Demokratic Party, UDP, kimewataka wabunge wa UKAWA kurerejea na kuhudhuria vikao vya Bunge kwani jukumu lao ni kuwawakilisha wananchi waliowachagua na kitendo cha kuendelea kususia Bunge ni sawa na kuwanyima haki watanzania.
Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tiafa wa UDP , Bw. ,John Cheyo, mara baada ya kuwapokea wanachama wapya 15 akiwemo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Goodluck Ole Medeye, ambaye amejiengua kutoka chama cha CHADEMA .
Kwa upande wake Dk. Olemedeye amesema, amepitia Katiba za vyama vingi vya siasa na kuridhishwa na Katiba ya UDP kwani imelenga kumkomboa mwananchi wa kawaida.