Ijumaa , 14th Feb , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Kenzo amesema kuwa, matumaini ya uhai wa muziki wake katika siku za mbeleni yapo katika giza nene, na hii ni baada ya hatua ya lebo ya Ogopa Deejayz kusitisha mikataba waliyokuwa nayo na wasanii wake hivi karibuni.

Kenzo amesema kuwa, amekuwa akifanyakazi zake zote akiwa chini ya Ogopa na amewafahamu kama familia yake, na baada ya kuwa nje ya lebo hii sasa amepoteza matumaini katika muziki wake kabisa.

Kenzo amesema kuwa, amejiona kama mtengwa na anatarajia pengine kutakuwa na mabadiliko ambayo yatasaidia kumtengenezea njia ya kumrudisha katika gemu.