Jumatatu , 6th Jun , 2016

Msanii Cyril kamikaze amefafanua mtafaruku uliojitokeza kati yake na uongozi wa WCB, baada ya kutoa wimbo aliomshirikisha Raymond na uongozi wake kusema hautambui collabo hiyo.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Cyril amesema alishangazwa na kauli ya meneja wa WCB Salaam SK kuwa hawaitambui collabo aliyofanya na raymond, na kumtuhumu huenda anatafuta kiki, kwa madai kuwa msanii huyo kwa sasa anafanya vizuri.

Kwa upande wake Cyril amesema wimbo huo uliandikwa na Raymond, na pia kuna verse aliimba lakini alilazimika kuitoa, baada ya mgongano huo kutokea, collabo ambayo kwa mujibu wake Cyril alirekodiwa muda mrefu kabla Raymond hajaingia wcb.

Tazama hapa interview nzima na Planet Bongo akiongelea suala hilo.