Jumamosi , 7th Mei , 2016

Vilabu 10 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania vimeanza mbio za kuwania ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa ya Taifa ambayo imeanza hii leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya ndani vya taifa na ABC vyote vya Dar es Salaam.

Moja ya timu shiriki katika ligi ya mpira kikapu taifa NBL ikikaguliwa kabla ya mchezo.

Ligi ya Taifa ya Klabu Bingwa ya Kikapu nchini Tanzania imekatwa utepe hii leo katika viwanja vya ndani wa taifa ikizikutanisha timu mbalimbali kutoka mikoa ya Dar es Salaam iliyoingiza timu tatu, Tanga, Arusha, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Rukwa na Mbeya.

Akizungumzia ligi hiyo ambayo inachezwa kwa makundi mawili ya A na B yenye timu tano tano kila kundi kamishina wa ufundi na uendeshaji mashindano wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF ambao ndiyo waandaaji wa ligi hiyo Manasseh Zablon Mghamba amesema ligi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote shiriki ambazo ndio mabingwa wa mikoa yao.

Aidha, Manase amesema kuwa TBF itatumia mashindano hayo kusaka vipaji vipya vyakuongeza katika timu ya taifa ambayo baadaye itashiriki katika michuano mbalimbali ya Kimataifa.

Katika mgawanyo huo wa makundi hayo mawili ya A na B ambayo yamepewa majina ya Pool kama ifuatavyo -:

POOL A
1 .JKT - DSM.
2.TPA-TANGA.
3. UDOM.- DODOMA.
4. VIJANA - DSM.
5 YOUNG WARRIORS - MORO.

POOL B
1. SAVIO - DSM.
2. KINGS - ARUSHA.
3. MARINE -MTWARA.
4. RUKWA STARS.
5 MBEYA FRAMES.