Jumatano , 13th Apr , 2016

Serikali imepanga kuwatawanya Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwapeleka katika Hospitali za rufaa za Mikoa kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi ambao wanashindwa kuzifuata jijini Dar es Salaam.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu,

Hayo yameelezwa na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu,alipofanya ziara Mkoani Mtwara, na kuongeza kuwa tayari ameshafanya nao mazungumzo juu ya mkakati huo ambapo wamekubali huku wakisisitiza uwepo wa vifaa tiba katika hospitali watakazo pelekwa kwa ajili ya kutolea huduma hizo.

Aidha, amewataka viongozi wa hospitali hizo pamoja na halmashauri husika kuandaa mazingira mazuri ya kuwavutia wataalamu hao kwa kuboresha makazi pamoja na mishahara kulipwa kwa wakati, ili wawe na morali nzuri ya kuwahudumia wananchi.

Mhe. Ummy ameongeza kuwa kuna Madaktari ambao wako tayari kufanya kazi wilayani lakini tatizo ni mazingira ya ufanyaji kazi ndio unakuwa mgumu kutokana na halmashauri nyingi kutokuwa na miundombinu rafiki ya wao kufanya kazi.

Sauti ya waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu,