Kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Isaya Mngulu
Jeshi la polisi nchini limetoa donge nono la shilingi milioni kumi kwa mwananchi yeyote atakayefichua mtandao wa watu wanaotengeneza na kulipua mabomu katika mikusanyiko ya wananchi vitendo ambavyo vimekuwa vikiuwa na kujeruhi wananchi wasio na hatia.
Hayo yamesema na kamshina wa makosa ya jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu alipokuwa akizungumza na waadishi wa habari jijini Arusha
Kuhusu hatua iliyofikiwa kuwatafuta watu waliohusika katika tukio la mlipuko wa bomu kwenye baa ya Night Park kamshna Mngulu amesema hawajapatikana na kwamba hata waliohusika kwenye matukio ya bomu katika kanisa la Olasiti na pia kwenye mkutano wa CHADEMA Soweto pia hawajapatikana japo amesema jitihada za kuwatafuta zinaendelea.
Katika hatua nyingine kamshina Mngulu amekiri kuwa changamoto bado ni kubwa katika kuwatambua watu wanaoendesha vitendo hivyo na ameendelea kuwaomba wananchi kusaidia kwa kutoa taarifa na kwamba hata ndani ya vyombo vya dola pia iko haja ya kujichunguza kwani haiwezekani vitendeo hivyo viendelee kutokea na wahusika wasipatikane.
Wakizungumzia vitendo hivyo baadhi ya wananchi wamelitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa hata kutoa taarifa za matukio ya milipuko ya mabomu kila inapotokea.
Siku ya tarehe 13/04/2014 majira ya saa moja na nusu ulitokea mlipuko katika baa ya Night Park iliyoko jijini Arusha uliojeruhi watu 17 likiwa ni tukio la tatu kutokea katika jiji la Arusha ambapo matukio mengine mawili ya milipuko ya mabomu yalitokea mwaka 2013