Jumanne , 15th Apr , 2014

Msanii wa muziki Mrisho Mpoto usiku wa kuamkia leo amefanya onyesho huko nchini Dubai katika sherehe kubwa ya ubalozi wa Tanzania nchini humo kusherekea miaka 50 ya muungano wa Tanzania na Zanzibar.

MwanaFA Mrisho Mpoto Dubai

Katika sherehe hii pia msanii wa muziki wa kizazi Kipya, Mwana FA pia alikuwepo na kupata nafasi ya kudondosha burudani ya kutosha katika sherehe hii iliyofanyika kwa lengo pia la kudumisha zaidi uzalendo wa taifa la Tanzania.

Sherehe hii imepata kuudhuriwa na wageni mbalimbali, wengi wao wakiwa ni Watanzania waishio huko Dubai.