Jumatatu , 14th Apr , 2014

Mwanamama Zari Hassan pamoja na baba watoto wake Ivan Ssemwanga wameendelea kurushiana vijembe na kutambiana baada ya kutengana, ambapo safari hii Zari ameamua kuonyesha mitandaoni picha zaidi akiwa na mpenzi mpya Farouk na maneno ya kumdiss Ivan.

Zari, Ivan na familia

Katika upande wa pili wa shilingi, Ivan naye safari hii ameamua kujibu mashambulizi kwa aina ya tofauti kwa kujitapa kuwa anatengeneza pesa nyingi zaidi, huku akinunua gari jipya la kifahari na kutangaza kuwa mama watoto wake huyu ameishiwa na hana kitu kwa sasa.

Wapenzi hawa ambao wamekuwa na historia ya kugombana na kutengana mara kadhaa sasa, safari hii kwa mujibu wa wachambuzi, wamefikia hatua mbaya kabisa ambayo inaashiria kua huenda huu ndio ukawa mwisho wa mahusiano yao kabisa.

Tags: