Jumatano , 2nd Mar , 2016

Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania (TANESCO),limewasilisha ombi la kutaka mabadiliko ya bei za Umeme kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura).

Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngalamgosi

TANESCO Imewasilisha Ombi hilo ikitaka mabadiliko hayo ya umeme kwa asilimia 1.1 kuanzia tarehe moja mwezi wa nne na asilimia 7.9 kwa mwezi January mwaka 2017.

Akitangaza kupokea maombi hayo Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amekiri kupokea ombi hilo na kusema kuwa kwa sasa wako kwenye utaratibu wa kukusanya maoni ya wadau ili waweze kufanya mabadiliko hayo kutoka na mabadiliko ya uzalishaji wa nishati hiyo nchini.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo ametangaza kushuka kwa bei ya nishati za mafuta ya taa, Petroli, na dizeli, baada ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia huku akisema mabadiliko hayo hayatahusu mkoa wa Tanga.

Akitangaza bei elekezi jijini Dar es Salaam Bw. Felix Ngamlagosi amewataka wateja wa nishati ya mafuta kudai risiti pindi wanapopewa huduma hiyo na kwamba kuanzia sasa wananchi wanaweza kupata bei hizo kupitia simu zao za kiganjani.