Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bariadi Mathias Mkumbo
Halmashauri hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu wa jumla ya madawati 6979, imejipanga vema kutekeleza agizo la mhe Rais na ifikapo Juni 31 kila mwanafunzi anasoma akiwa amekaa katika dawati.
Akizungumza katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bariadi Mathias Mkumbo, amesema kuwa halmashauri imeweka mkakati madhubuti wa kuwahamasisha wadau mbalimbali wa elimu wa kuchangia kwa hiari ili kuwawezesha kutatua kero za wanafunzi za kukaa chini ikiwa ni moja ya agizo la Rais la utekelezaji ifikapo Juni 31.
Kwa upande wao madiwani wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bariadi, Robert Rweyo wameahidi kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha elimu ngazi ya msingi na sekondari hadi vyuo vikuu kwani bila kuwepo na madawati kunaweza kuwakatisha tamaa baadhi ya watoto kuendelea na masomo hivyo ni fursa ya pekee kwa jamii kulipa suala hilo kiupaumbele.