Jumatatu , 3rd Feb , 2025

Mwanamke mmoja Raia wa nchini Marekani, Onijah Andrew Robinson, amezua taharuki mjini Karachi, Pakistan baada ya kudai dola 5,000 kwa wiki na kuelezea nia yake ya kuwa raia wa Pakistan kufuatia kuachwa kwenye mataa na mwanaume raia wa Pakistan waliyepanga kufunga ndoa.

Mwanamke mmoja Raia wa nchini Marekani, Onijah Andrew Robinson, amezua taharuki mjini Karachi, Pakistan baada ya kudai dola 5,000 kwa wiki na kuelezea nia yake ya kuwa raia wa Pakistan kufuatia kuachwa kwenye mataa na mwanaume raia wa Pakistan waliyepanga kufunga ndoa.

Robinson, (33) alisafiri kwenda Pakistan mnamo Oktoba 2024 ili kumuoa Nidal Ahmed Memon mwenye umri wa miaka 19, baada ya wawili hao kudaiwa kuingia kwenye uhusiano wa mtandaoni. Hata hivyo, alipowasili, Memon, chini ya shinikizo kutoka kwa familia yake, alikataa kumuoa, na kumuacha Robinson akiwa amekwama Karachi.

Akiwa na visa ya utalii iliyoisha muda wake na kukosa mahali pa kukaa, Robinson alienda nyumbani kwa Memon katika eneo la Bustani, na kukuta familia ya kijana huyo ilikuwa imeiondoka kwenye nyumba hiyo.

Akiwa amekata tamaa na bila msaada, Mwanamke huyo aliamua kufanya makazi na kuchukua hifadhi katika eneo la maegesho ya nyumba hiyo. jambo ambalo limevutia hisia za wakaazi na wapita njia wa eneo hilo na kusababisha kuongezeka kwa wasiwasi juu ya usalama.

Katika hali ya kushangaza Robinson amenukiliwa akiwaambia maafisa wa serikali ya Pakistan kuwa "mnapaswa kunipa dola 5000 kwa wiki, Mimi ni raia wa Pakistan." alitishia zaidi kutoondoka isipokuwa matakwa yake yatimizwe na kukataa katakata kurudi nchini kwake licha ya msaada kutoka ubalozi wa Marekani wa tiketi ya kurudi

Hata hivyo kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jeremiah Robinson mtoto wa mwanamke huyo amesema ya kuwa mama yake ana matatizo ya akili na walishafanya juhudi za kumrudisha Marekani yeye pamoja na kaka yake pasipo mafanikio