Jumatatu , 3rd Feb , 2025

Mwili wa mchimbaji mmoja kati ya watatu waliofukiwa na kifusi baada ya duara kumeguka katikati kwenye mgodi wa Nkandi eneo la Mwime, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga waopolewa. 

Mwili wa mchimbaji uliotolewa ndani ya kifusi

Zoezi la uokoaji bado linaendelea kwa ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kahama.

Wachimbaji watatu wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Nkandi uliopo eneo la Mwime, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, walifukiwa na kifusi hicho Februari Mosi mwaka huu wakati wakiendelea na shughuli zao za uchimbaji.