Jumanne , 4th Feb , 2025

Muungano wa makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza usitishaji mapigano wa kibinadamu kuanzia Jumanne.

Muungano wa makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza usitishaji mapigano wa kibinadamu kuanzia Jumanne.

Katika taarifa ya kundi hilo linalojumuisha waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda lilitaja "sababu za kibinadamu" za kusitisha mapigano, baada ya kuteka maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 900 wameuawa na wengine 2,880 kujeruhiwa katika mapigano ya hivi majuzi katika na karibu na Goma, mji mkubwa wa mashariki mwa DRC, baada ya kutekwa na waasi.

Mataifa ya G7 na EU yamelaani mashambulio hayo kama ukiukaji wa wazi wa uhuru wa DR Congo huku Muungano wa makundi ya waasi unaojulikana kama Muungano wa Mto Congo umeshutumu jeshi la Kongo (Congo River Alliance) -kwa kuua watu wakitumia ndege kupiga mabomu maeneo wanayoshikilia.

Iliongeza kuwa haina nia ya kunyakua eneo lolote zaidi, licha ya kusema vinginevyo wiki iliyopita, na itashikilia misimamo yake, Katika taarifa, muungano huo ulisema: "Tunasisitiza dhamira yetu ya kulinda na kutetea raia na nafasi zetu."

Mapigano ya kikanda yameshuhudia mamia ya maelfu ya watu wakihama makazi yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Tangu kuanza kwa 2025, zaidi ya watu 400,000 wamelazimika kutoka kwa makazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.