Jumapili , 7th Feb , 2016

Msanii wa Filamu kutoka nchini Kenya anaefanya kazi zake nchini Ujerumani Ashley Toto, amezindua kampuni yake ya Ashley Toto Media(ATM) ambayo ni kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa Afrika na kuwainua wasanii wa Afrika Mashariki na kati.

Msanii wa Filamu kutoka nchini Kenya, Ashley Toto,

Ashley amesema amehamasika kufungua kampuni hiyo baada ya kuona watoto wengi nchi za kiafrika wanapata tabu kutimiza ndoto zao, hivyo kupitia kampuni hiyo kuna uwezekano wa kuwasaidia ili kutimiza malengo yao..

Aidha amesema atajihusisha na kuwasaidia wasanii wa Afrika Mashariki kufanya show za kimataifa ikiwemo Ujerumani, pamoja na nchi nyingine za Scandnavia ili kuupeleka muziki wa Afrika Mashariki mbali zaidi.