Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Mkurugenzi msaidizi magonjwa yasiyoambukizwa katika Wizara ya Afya nchini, Profesa Ayoub Magimba amesema kuwa mpango huo umewezeshwa na ubia wa chanjo duniani, GAVI..
Amesema hatua nyingine ni huduma ya matibabu kwa njia ya mionzi ya nyuklia ili kubaini na kutibu saratani itakayotolewa katika mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma..
Nchini Tanzania idadi ya wagonjwa wapya wa saratani kila mwaka inakadiriwa kuwa elfu 44 ambapo hata hivyo wanaoweza kufika hospitali kusaka huduma ni asilimia 10 pekee, wengi wao wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa huo.