Ijumaa , 29th Jan , 2016

Msanii Q Chief ambaye sasa yupo chini ya Bendi mpya ya Q S Mhonda, ameeleza kuwa licha ya uzoefu wake katika muziki kwa miaka, amejiweka pembeni na jukumu la kuongoza bendi hiyo mpya kutokana na lawama nyingi ambazo huambatana na nafasi hiyo.

Q chief amesema kuwa, anasaidia bendi yake hiyo kwa kuwakutanisha na wasanii na wadau mbalimbali kuwapa semina wasanii ambao atakuwa akifanya nao kazi katika bendi hiyo ambayo itazinduliwa rasmi kwa tukio kubwa la onyesho la burudani jumapili hii.

Akizungumzia uzoefu wake, Q Chief amesema kuwa kuishi na wanamuziki kunahitaji moyo, akiwa sasa amekwishaweka mambo yake sawa tayari kwa kuendesha shughuli zake na bendo hiyo, jukumu ambalo atalifanya sambamba na safari yake kama "Solo Artist'.

Tags: