Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na katibu wa halmashauri kuu ya Taifa, itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya mwanasheria wa Chadema Tundu lissu kwamba agenda ya kupinga ufisadini ya chama chao na Rais Magufuli hataweza kuikomesha kutokana na mfumo wa CCM.
''Kama kweli chama hicho cha upinzani kina nia ya dhati ya kuitekeleza ajenda hiyo ni vyema wakajitokeza hadharani na kumuunga mkono Dk Magufuli, ambaye ameonesha si tu kwa kulizungumzia ajenda hiyo ya kupambana na ufisadi, bali anaitekeleza kwa vitendo''Amesema Nape.
Nape ameongeza kuwa hatua ya Rais imepongezwa na Watanzania wengi pamoja na jumuiya za kimataifa kwa jinsi anavyoshughulikia suala la kupambana na ufisadi, huku akisisitiza kuwa nia ya serikali yake ni kuwajali Watanzania wanyonge ili wafaidi rasilimali za nchi yao.


