Jumatano , 13th Jan , 2016

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limetangaza kuanza rasmi zoezi la kuwasaka na kuwakamata madereva wa bodaboda wanaohusishwa na tuhuma za wizi wa kutumia pikipiki na kufanya makosa mengine ya kihalifu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kuanza rasmi zoezi la kuwasaka na kuwakamata madereva wa bodaboda wanaohusishwa na tuhuma za wizi wa kutumia pikipiki na kufanya makosa mengine ya kihalifu.

Akiongea leo jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa hadi sasa tayari jeshi hilo limejipanga kudhibiti uhalifu jijini kwa kuwakamata wahalifu waliohusishwa na makosa ya wizi wa kutumia pikipiki ikiwa ni pamoja na kuua kwa kutumia silaha.

Aidha, Kamanda Sirro amesema kuwa jeshi hilo pia litafanya msako wa kuwakamata wanawake wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwani wamekuwa wakishirikiana na wahalifu kufanya vitendo vya kihalifu.