Jumatatu , 4th Jan , 2016

Mwanamuziki wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania aliyewahi kutamba na Bendi ya Twanga Pepeta Dogo Rama ambae sasa ameibukia Bendi ya Double M Plus, amesema mashabiki wake wawe tayari kwa kibao kikali cha 'Mapungufu Yangu'.

Mwanamuzi wa Muziki wa Dansi nchini Dogo Rama

Dogo Rama ambaye album yake ya Kilometa 10,000 ilifanya vizuri amesema kwa sasa ameandaa wimbo kwa ajili ya band yake mpya, lakini bado yupo kwenye mchakato wa kukamilisha album yake nyingine ya Kilometa Part 2.

Dogo Rama amesema wimbo wa 'Mapungufu Yangu' una ujumbe tofati na nyimbo nyingi za sasa ambazo zimejaa mapenzi wakati kuna maisha mengine zaidi ya mapenzi.