Jumamosi , 2nd Jan , 2016

Nahodha wa zamani wa klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza Steven Gerrard anataraji kurudi kwenye klabu hiyo kama kocha pindi atakapomaliza kusukuma ngozi kwenye klabu ya L.A Galaxy ya nchini Marekani.

Gerrard mwenye umri wa miaka 35,ambaye alishinda mataji 10 katika klabu ya Liverpool,amesema amefanya mazungumzo na kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp na amemkaribisha kufanya naye kazi.

Gerrard ambaye mkataba wake na LA Galaxy unamalizika mwishoni mwa mwaka huu,amesema anataraji kurudi Uingereza miezi ya Novemba na Desemba ambapo atasomea ukocha,vile atakuwa na kazi ya kuzunguuka katika timu mbali mbali ili kupata uzoefu wa kazi hiyo na mahusiano mazuri na mameneja.