
Kikosi cha Nanda fc katika picha ya pamoja kabla ya moja ya mechi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara .
Msemaji wa wanakuchele hao Idrissa Bandari ameiambia East Afrika Radio kuwa hatua hiyo inakuja kufuatia timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya msimu huu ambapo imefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu kati ya 12 mpaka sasa wakiwa nafasi ya 13 kwa alama zao sita.
Kikosi cha Ndanda Kilikumbana na kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa maafande wa Jkt Ruvu wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Nangwanda Sijaona hali iliyoleta sintofahamu ndani ya timu hiyo iliyonusurika kuporomoka daraja msimu uliopita.
Timu hiyo ipo kwenye wakati mgumu zaidi kutokana na ratiba ya ligi hiyo ambayo inaonyesha itaumana na wekundu wa msimbazi simba katika mechi ya kiporo itakayopigwa kati kati ya juma hili.