Jumanne , 22nd Dec , 2015

Kocha Mkuu wa JKT Ruvu Abdallah Kibaden amesema atahakikisha anafuta makosa yaliyomsababishia asipate ushindi dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara uliochezwa juzi uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Kibaden amesema, atafanya marekebisho makubwa katika kikosi chake ili kumwezesha kupata matokeo mazuri dhidi ya Ndanda FC katika mchezo utakaopigwa Jumamosi uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara.

Kibaden amesema wachezaji wake walishindwa kupata matokeo mazuri kutokana na upungufu uliojitokeza katika idara mbalimbali ikwemo ulinzi.

Kibaden amesema, mabeki wake walikosa umakini wa kucheza na washambuliaji wa Coastal Union na kusababisha kuruhusu mabao ambayo walifungwa kwenye mchezo huo.

Kibaden amesema, baada ya kubaini upungufu huo, anatarajia kuyafanyia kazi kabla ya kukutana na Ndanda FC ambapo wanatarajia kuondoka hapo kesho tayari kwa mchezo huo.

Kibaden amesema, pamoja na kutoka sare katika mchezo huo lakini wachezaji wake wanaonekana kubadilika tofauti na alivyoikuta timu.