Ijumaa , 11th Dec , 2015

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi amesema Tanzania inakabiliwa na uhaba mkubwa wa madaktari na wauguzi, hivyo ameishauri serikali kufanya jitihada kubwa kuhakikisha inaziba pengo hilo ili kuokoa maisha ya wananchi.

Rais wa Awamu ya pili nchini Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi,

Mzee Mwinyi ameyasema hayo jana katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afya na Teknolojia (IMTU), yaliyofanyika chuoni hapo ambapo wahitimu 148 walitunukiwa shahada ya udaktari.

Aidha Mzee Mwinyi ameongeza kuwa baadhi ya nchi daktari mmoja anahudumu wagonjwa wachache kwa wakati mmoja wakati daktari wa Tanzania anahudumia maelfu ya watu hivyo kufanya huduma ya afya kuzorota.

Hata hivyo alisifu juhudi zinazofanywa na IMTU, kuzalisha wahitimu wa udaktari na uuguzi ikiwa ni mchango wake kwa serikali wa kupunguza pengo hilo la uhaba.