Jumamosi , 5th Dec , 2015

Kufuatia malalamiko kadhaa juu ya mahusiano mabovu kati ya wasanii wa kike hapa Bongo, diva wa muziki Baby J ametoa wito kwa wasanii wenzake kuunganisha nguvu na kuwa na umoja kutokana na kazi wanayofanya kutegemea sana ushirikiano ili kusonga mbele.

Baby J

Baby J ambaye kwa sasa anaendesha muziki wake akiwa chini ya Mkubwa na Wanawe, pia akaeleza kuwa kwa roho iliyokunjuka kabisa, wasanii wenzake wanatakiwa kujifunza na kumtazama kama mfano, Vanessa Mdee staa ambaye ameweza kupiga hatua kubwa kimuziki, eNewz ikiwa na za chini ya carpet juu ya kuwepo kwa kolabo kati ya wasanii hawa wawili njiani.

Baby J anayewakilisha poa kutoka visiwa vya Zanzibar, sambamba na maneno hayo amekazia kuwa, mafanikio ya mtu ni nafasi ya kujifunza na si kukunja na kuoneana wivu, kitu ambacho kinarudisha muziki nyuma kwa kiasi kikubwa.

Tags: