Jumatano , 2nd Dec , 2015

Maziko ya dogo aliyejijengea umaarufu kupitia dansi ya rekodi maarufu ya 'Sitya Loss' huko Uganda, Alex Ssempijja yamefanyika leo huko Kibibi, Butambala katika kitongoji cha Mpigi, baada ya kupoteza maisha juzi kwa ajali ya baiskeli.

dogo aliyejijengea umaarufu kupitia wimbo wa 'Sitya Loss' huko Uganda, marehemu Alex Ssempijja

Marehemu ambaye alikuwa na umri wa miaka 13 tu, akiwa na ndoto kubwa za kuibadilisha dunia kupitia dansi, anagusa wengi kupitia msiba huo akimuacha dansa mwenzake Patricia Nabakooza akiwa majeruhi kutoka katika ajali hiyo hiyo.

Wakati haya yakiendelea wazushi tayari wameibuka na kumhusisha staa wa muziki Eddy Kenzo kuhusika na kifo cha kinda huyo kwa imani za kishirikina, taarifa ambazo mpaka sasa Kenzo bado hajataka kuzizungumzia kwa namna yoyote.