
Kapombe amesema, marekebisho yatafanyika ndani ya siku moja kwakuwa kocha ameshaona mapungufu katika mchezo wa kwanza ambao walitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 2-2 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kapombe amesema, katika mchezo wa kwanza walifanya makosa ambayo yalichangia kutoka sare lakini kwa marekebisho yatakayofanywa na kocha wana uwezo wa kuibuka na ushindi katika mchezo wa marudiano na kuweza kusonga mbele.
Kapombe amewataka watanzania kuendelea kuwa nyuma yao kwa kuwapa sapoti ili kuweza kuipeperusha bendera ya nchi katika mchezo huo na kuweza kupangwa katika makundi.
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani hapo kesho nchini Algeria kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Algeria kwa ajili ya kuwania teketi ya kuweza kupangwa katika hatua za makundi ya kombe la dunia litakalofanyika 2018 nchini Urusi.