Jumatatu , 16th Nov , 2015

Mkali wa muziki wa rap Nikki Mbishi, amesema kuwa wasanii wa muziki wanaosikika katika radio, na vilevile kuingia katika vinyanganyiro vya tuzo na hata kushinda, sio wasanii wa hip hop, bali wanatembelea tu kivuli cha muziki huo.

Mkali wa muziki wa rap nchini Tanzania Nikki Mbishi

Maneno hayo ya Nikki ambayo yanaonekana kuwa ni kuwadiss kundi fulani la wasanii wa hip hop, ameeleza kuwa akiwa kama mwana hip hop anakerwa sana na suala hilo akiona watu wengine wanatengeneza pesa kwa kutumia kile anachokiita kivuli cha muziki huo.

Rapa huyo kwa hisia nzito, anaeleza hapa mwenyewe juu ya hili.